BODI YA USHAURI SRRH YATEMBELEA KITENGO CHA TIBA MTANDAO

Posted on: November 30th, 2023


Na SRRH

BODI ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Shinyanga, katika kikao chake cha tano ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Dkt. Frank Samwel, ilitembelea Kitengo cha Tiba Mtandao (Telemedicine) na kupokea maelekezo ya namna kinavyofanya kazi kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali, Dkt. Luzila John.

Katika ziara hiyo, Bodi iliipongeza Serikali inayooongozwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha huduma za tiba mtandao, kwani itarahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa bila kusafiri umbali mrefu kupata huduma hizo.

Aidha, katika kuboresha huduma za afya, Serikali imeanzisha huduma hiyo katika Hospitali za Rufaa za mikoa, Hospitali za Kanda, Hospitali Maalumu na Hospitali ya Taifa.

Kutokana na huduma ya Tiba Mtandao, mgonjwa anaweza kuonwa na kupata matibabu katika Hospitali A na Madaktari kutoka Hospitali B kwa kupitia Tiba Mtandao.