KLINIKI YA KIBINGWA YA MAGONJWA YA KOO, PUA NA MASIKIO KUFANYIKA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SHINYANGA
Posted on: January 30th, 2026
Na Shinyanga RRH
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga inautaarifu umma kuwa itaendesha Kliniki ya Kibingwa ya Magonjwa ya Koo, Pua na Masikio (ENT) kuanzia tarehe 2 Februari hadi 13 Februari, 2026.
Kliniki hiyo itaendeshwa na Daktari Bingwa wa Koo, Pua na Masikio, na itahudumia wagonjwa wenye matatizo mbalimbali ya koo, pua au masikio, pamoja na watoto wanaosumbuliwa na kukoroma, kupumua kwa shida, kuvimba kwa tezi za koo na nyama za pua.
Wananchi wote wenye changamoto hizo wanahimizwa kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya kitaalamu kwa wakati.


