MGANGA MKUU SHINYANGA, KATIBU TAWALA KISHAPU WALA KIAPO CHA AHADI YA UADILIFU KWA VIONGOZI WA UMMA

Posted on: October 25th, 2023


Na SRRH

MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Yudas Lucas Ndungile, na katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Bi. Fatma Mohamed, wamekula kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Vingozi wa Umma mbele ya Katibu Msaidizi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Umma kanda ya Magharibi, Gerald Mwaitebele, katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Katika zoezi hilo lililofanyika Oktoba 25, 2023, Katibu Mwaitebele alitoa maelekezo ya kwenda kutekeleza majukumu ya kazi kwa uadilifu, pamoja na kuzingatia maslahi ya wananchi ambao ndiyo walengwa wakuu wanaopaswa kuhudumiwa.

"Dr. Yudas Lucas Ndungile, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Mkoa wa Shinyanga na Bi. Fatma Mohamed Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu mmeapa hapa.

“Muende sasa mkawe msaada kwa wananchi, hao ndiyo walengwa wakuu mnaopaswa kuwahudumia vizuri, kumbukeni kuwa cheo ni dhamana"

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza D. Tumbo, alisisitiza kwa kuwaeleza viongozi waliokula kiapo kufanya kazi kwa kutanguliza uzalendo na kwa ufasaha.

"Nendeni mkatangulize uzalendo katika majukumu yenu ya kazi, uadilifu ni kitu muhimu zha kuzingatia, mchape kazi kwa bidii", alisema Prof. Tumbo.