WATUMISHI HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA WAPATIWA MAFUNZO YA CHATI UCHUNGU

Posted on: December 28th, 2023


Na SRRH

WATUMISHI wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wamepatiwa mafunzo ya Chati Uchungu (Labour Care Guide) inayosaidia kujua maendeleo ya Mama mjamzito pamoja na mtoto tumboni kabla ya kujifungua.

Mafunzo hayo yanayofanyika kwa siku tano (5) yameanza kuwezeshwa kuanzia Jumanne ya Disemba 26, 2023 na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya akina Mama na Uzazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Shinyanga, Agustino Maufi, pamoja na Muuguzi Msaidizi, Wile Dadi ambao walipata mafunzo maalumu kutoka kwa wataalamu wa Wizara ya Afya.

Mafunzo ya Chati Uchungu yakifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hospitali ya Rufaa Mkoa Shinyanga.

Ujio wa mafunzo haya yanayofanyika nchi nzima umesababishwa na maboresho ya hii Chati Uchungu mpya, tofauti na ile ya awali ambayo ilionekana kuwa na mapungufu.

Chati Uchungu mpya na iliyoboreshwa itakuwa inatumika katika vituo vyote vya Afya na Hospitali zote nchi nzima.